Wednesday, May 9, 2012

KICHEKESHO:
Bosi moja alikwenda kwenye mkutano, kiongozi mmoja akaanza mkutano kwa kichekesho, Akasema,'Sehemu kubwa ya maisha yangu nilipata furaha toka kwa mwanamke ambaye hakuwa mke wangu', watu wakati wanashangaashangaa akamalizia, 'Mwanamke mwenyewe ni mama yangu', watu wakacheka sana.
Siku moja kukawa na pati ya wafanyakazi na familia zao bosi akiwa ameshaweka kinywaji akaamua kurudia kile kichekesho kufurahisha wafanyakazi wake. Akaanza, 'Sehemu kubwa ya maisha yangu nilipata furaha toka kwa mwanamke na mwanamke huyo hakuwa mke wangu' Mke wa bosi hapo hapo akaguna 'Ughhh', Jamaa kwa ajili ya pombe akawa amesahau kichekesho kilikuwa kinamalizika vipi,'Akaishia halafu mwanamke mwenyewe simkumbuki'...................